jumuiya hii inawalezi nje na ndani ya chuo walezi wandani wakiwemo ukhut mariyam kuhenga, anzuruni nawengineo walezi wa nje akiwemo ust: mohamed immamu wa masjd feri, issa othumani imam musjid maamur upanga viongozi walizi hawa ndio wana saidia kupeleka gurudumu hili mbele na kuhakikisha kila kitu kiko sawa
madhumuni
1 kuandaa wanafunzi kuwa katika maadili ya kidini
2 kuwaandaa kuwa watumishi wazuri wa umma wa kiislam
3 kujenga umoja, kufahamiana na mshikamana
malengo
kuifanya jumuiya yetu itambulike na iwe na mchango mkubwa katika wasomi wa sasa wa kiislam na jamiii kwa ujumla
hiyo ndio TMUSA Kwa muhtasali
mafunzo
Mwanaadamu
Nani Mwanaadamu? Nani wewe na
nani mimi? Kwa nini tupo hapa katika ardhi. Haya ni maswali muhimu
sana, hasa baada ya kutoa maelezo juu ya Allah. Kumzungumzia Mwanaadamu
kwa kumuhusisha na Allah (s.w.) ni eneo jingine linalohitaji kufahamika
vyema ili kuifanya midahalo kati ya Waislamu na wasio Waislamu, hasa
Wakristo, iwe yenye maana.
Qur’an inatufahamisha kwamba sisi Wanaadamu tumeumbwa kwa vitu vitatu.
Kwanza, tumetokana na udongo ambao unawakilisha umbile la mwili. Pili,
tumetunukiwa akili na kipawa cha kufikiri (Intellect) ambacho hakina
budi kutumiwa na Mwanaadamu.
Akili inaweza kuwa si toshelevu lakini vile vile si kikwazo cha imani. Na tatu, tumepuliziwa roho inayotokana na Allah:
Ambaye ametengeneza umbo la kitu, na akaanzisha umbo la mwanaadamu kwa udongo.
Q32:7
Katika aya nyingine Allah analiweka wazi zaidi hili kwa kutufahamisha:-
"Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia
Malaika, "Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti,
wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda."
"Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana na Mimi, basi mumwangukie kwa kumtii.
Q15:28-29
Kwa hiyo, Muislamu hayaoni maisha ya Mwanaadamu hapa ardhini kama ni
adhabu iliyotokana na wazazi wetu wawili Adamu na Hawa kula tunda la mti
uliokatazwa. Bali tukio hilo kihistoria linaitakidiwa kuwa ni fundisho
kwa Adamu na Hawa kabla ya kuletwa hapa duniani. Hili ni eneo jengine
lenye ukinzani.
Qur’an inafundisha kwamba hata kabla kumuumba mtu wa kwanza, Allah
(s.w.) alikusudia kuanzisha maisha na ustaarabu wa kiumbe huyu hapa
ardhini.
"(Wakumbushe watu khabari hii) wakati Mola wako alipowaambia Malaika: "Mimi nitaleta khalifa katika ardhi.".
Q2:30
Hii ina maana kwamba Muislamu haikubali dhana ya dhambi ya asili
iliyorithiwa kutoka kwa wazazi wao kwa kuasi amri ya Mwenyezi Mungu ya
kutokula tunda la mti uliokatazwa.
Allah amemuumba mtu ili aje kuwa Khalifa; mdhamini au mwakilishi wa
Allah katika ardhi. Dhamana aliyobeba Mwanaadamu na jukumu lake kwa
kujumla kwa Muumba (Allah) ni kumuabudu.
Ibada kwa Muislamu haikomei katika kutekeleza kaida fulani fulani
(rituals). Ibada katika Uislamu ina tafsiri pana; ni kuiendea shughuli
yoyote yenye manufaa kwa mtu binafsi au jamii kwa ujumla kwa mujibu wa
maelekezo ya Allah (s.w.).
Kwa maana hii, Muislamu anaitazama ardhi, mazingira na rasilimali zake
kama ni neema kutoka kwa Allah kwa Mwanaadamu ambayo anapaswa kuitumia
ili kufikia utimilifu wa amana (lengo) atakayowajibika kwayo mbele ya
Muumba. Hii ndiyo sababu kubwa Qur’an kusisitiza kusoma, kama
inavyojitokeza katika Wahyi wa kwanza:
"Soma kwa jina la Mola wako
Aliyeumba. Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha
(Binaadamu) kwa wasitu wa kalamu. Amemfundisha Mwanaadamu mambo
aliyokuwa hayajui".
Q96:1-5
Hivyo, kwa kuwa Waislamu huko nyuma walikuwa na yakini juu ya imani yao,
na juu ya maamrisho ya Qur’an kuhusu kusoma, walianzisha na kusimamia
ustaarabu na taaluma za sayansi zilizopea. Walirithishana na kuziboresha
hazina hizo ambazo baadaye zikaja kuwa cheche za mwamko wa Ulaya.
Tungependa kusisitiza hapa kwamba iwapo Waislamu wa zama hizi watakuwa
wakweli katika imani yao, historia ile itajirudia.
Wale wote woga hawako tayari kulipokea dai hili na kwa hiyo wanaogopa
mdahalo na hilo linathibitisha utukufu wa Uislamu. Bila shaka ndilo
umbile aliloumbiwa kwalo Mwanaadamu:
"Basi uelekeze uso wako katika dini
iliyo sawa sawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowambia watu. Hakuna
mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini
iliyo ya khaki lakini watu wengi hawajui. q30:30
BY BUSAZI HAMISI
0713130507
Amir wa tekinolojia habari na mawasiliano TMUSA
BY BUSAZI HAMISI
0713130507
Amir wa tekinolojia habari na mawasiliano TMUSA
Q30:30
AMIIN
ReplyDelete